Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA imeanza mkutano wa kutathimini kazi zake

IAEA imeanza mkutano wa kutathimini kazi zake

Zaidi ya wajumbe 1400 kutoka sehemu mbali mbali dunini wamekusanyika mjini Vienna nchini Austria kwenye mkutano mkuu wa kila mwaka wa shirika la umoja wa mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA .

Kati ya ajenda kwenye mkutano huo wa siku tano ni pamoja na uwezo wa kinyuklia wa taifa la Israel pamoja na uwezo wa shirika hilo katika eneo la mashariki ya kati.

Katibu mkuu wa mkutano huo Kwaku Aning amesema kuwa mkutano huo utatathimini yaliyojiri mwaka huu na mipango ya siku za baadaye . Mkutano huo pia kwa upande mwingine utawavutia wataalamu wa hali ya juu kutoka pembe zote za ulimwngi.

(SAUTI YA KWAKU ANING)