Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa kibinadamu Somalia unapunguka lakini watu milioni 2 baado wahitaji msaada

Mzozo wa kibinadamu Somalia unapunguka lakini watu milioni 2 baado wahitaji msaada

Idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu huko Somalia imepunguka kwa asili mia 25 kufikia watu milioni 2 mnamo miezi 6 iliyopita.

Hali hiyo inapunguza mzigo mkubwa kwenye moja wapo ya huduma za dharura zilizokumbwa na mzozo duniani . Hii ni kufuatana na utafiti ulochapishwa Jumatatu na kitengo cha usalama wa chakula na lishe cha Idara ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa FAO.

Uchunguzi unaonya kamba ingawa Somalia imeweza kupata mvua nyingi kupita kiwango cha kawaida, lakini bila ya kuimariasha uzalishaji chakula na ufugaji mifugo basi mafanikio yaliyopatikana yanaweza kutoweka mara moja.

Hali ya hivi sasa inaashiria mafanikio mazuri lakini kutokana na asili mia 27 ya wasomali wakiwa bado na mahitaji makubwa ya dharura basi hali itaendelea kua tete.

.