Skip to main content

UM unaonya hali kusini mwa Pakistan huwenda ikazorota zaidi wakati huduma zinaendelea kuimarika

UM unaonya hali kusini mwa Pakistan huwenda ikazorota zaidi wakati huduma zinaendelea kuimarika

Hali ya huduma za dharura inaendelea kua ngumu huku jimbo la kusini la Sindh linatajwa hivi sasa kua ndilo jimbo lililoathrika vibaya sana na mafuriko huko Pakistan.

Watu wengi zaidi wanaendelea kuathirika na wasi wasi unaongezeka wakati maji ya mto Indus yakiendelea kupanda na kutishia miji mikubwa ya kusini na mafuriko zaidi.

Afisa wa Habari wa OCHA Maurizio Giuliano anasema "Ikiwa hawatoweza kuwafikia wale wenye mahitaji ya dharura, wanadhani kwamba magonjwa yanayotokana na maji yataenea, upungufu wa chakula na ukosefu wa makazi."

Anasema wanahofia kutazuka wimbi la pili la vifo katokana na magonjwa yanayotokana na maji. Huduma za dharura zimeanza kupata kasi katokana na fedha zilizoahidiwa kufika.