Skip to main content

Quartet imetoa wito wa Israel na Palestina kuanza mazungumzo ya ana kwa ana

Quartet imetoa wito wa Israel na Palestina kuanza mazungumzo ya ana kwa ana

Taarifa iliyotolewa na kundi la pande nne kwa ajili ya mashariki ya Kati Quartet linalojumuisha Umoja wa Mataifa, Urusi, Marekani na muungano wa Ulaya inasema inaunga mkono mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Israel na Palestina ili kupata suluhu ya kudumu ya amani.

Kundi hilo limesema linaendelea na msimamo wake wa kuhakikisha linajidhatiti kusaidia kupatikana kwa suluhisho la kudumu kama walivyoafikiana na kutoa taarifa yao June 26 na Septemba 24 mwaka 2009 mjini New York na Machi 19 mwaka huu mjini Moscow ambapo taarifa zote hizo zinachagiza majadiliano ya moja kwa moja kati ya Israel na Palestina.

Limesema hii itasaidia kutatua mambo muhimu na kumaliza kukaliwa kwa Palestina kulikoanza mwaka 1967 na hatimaye kuundwa kwa taifa huru na la kidemokrasia la Palestina na hivyo kuishi kwa amani na usalama na Israel pamoja na jirani zao wengine.

Quartet imtoa wito kwa Israel na Palestina kuhudhuria uzinduzi wa majadiliano ya ana kwa ana Septemba pili mwaka huu mjini Washngton na kutekeleza matakwa ya pande zote. Na imesema iko tayari kuzisaidia pande zote kwa wakati wote wa mazungumzo hayo.