Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zinazostahili kukabili majanga hazichukuliwi:ISDR

Hatua zinazostahili kukabili majanga hazichukuliwi:ISDR

Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mikakati ya kimataifa kwa ajili ya kupunguza majanga ISDR kinasema mabadiliko ya hali ya hewa ni chanzo kikubwa cha majanga mengi ya asili .

Kitengo hicho kinasema hilo limethibitika kutokana na majanga ya hivi karibuni kama mafuriko ya Pakistan, maporomoko ya udongo Uchina, moto wa msituni Urusi na ukame uliofurutu ada nchini Niger. Na kama anavyofafanua mkutugenzi wa sekretariati ya UNISDR Salvano Briceno hatari kwa maisha ya binadamu imeongezeka lakini serikali na jamii hazichukui hatua zinazostahili kushughulikia hali hiyo.

(SAUTI YA SALVANO BRICENO)

Silvano ameongeza kuwa ni wazi matukio ya miezi ya karibuni yanadhihirisha kwamba kuna umuhimu wa kuliangalia suala la kupunguza majanga kwa kina. Amesema ujumbe muhimu ni kwamba ingawa mabadiliko ya hali ya hewa ni chachu lakini kuna sababu nyingine pia zinazochangia ambazo zinahitaji kuchukuliwa hatua kama vile makaazi ya binadamu.