Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua muongo mzima wa vita dhidi ya ukame na jangwa duniani

UM umezindua muongo mzima wa vita dhidi ya ukame na jangwa duniani

Wadau wa kukabiliana na ukame na jangwa wametoa wito wa kuongezwa uelimishaji na mawasiliano katika maamuzi ya kuchukua hatua za kutokomeza uamasikini na kuchagiza maendeleo endelevu katika maeneo yenye ukame.

Jana Jumatatu muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa ulizinduliwa kwa lengo la kupata matokeo ya kukabiliana na hali ya ukame na jangwa.  Mkuu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na jangwa Gnacadja ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kwamba changamoto ni kuwafikia wanaofanya maamuzi ili kutoa kipaumbele cha suala hili katika ajenda ya maendeleo.

Ameongeza kuwa pia kuhakikisha kwamba ushirikiano wa kimataifa unaongezwa ili kuongeza rasilimali zaidi kwa maeneo yenye ukame na waweze kupambana na umasikini. Amesema tunajua hilo linawezekana.

Nakumbuka kwamba asilimia 50 ya mifugo ya dunia inatoka maeneo makame. Na asilimia 44 ya mfumo wa uzalishaji wa chakula unatoka maeneo makame. Zaidi ya watu 2000 wako Fortaleza Brazili kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu udhibiti wa hali ya hewa na maendeleo ya maeneo makame.