Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tiba ni moja ya chanzo kikubwa cha matumizi ya mionzi:UM

Tiba ni moja ya chanzo kikubwa cha matumizi ya mionzi:UM

Ripoti ya kamati ya sayanzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu athari za mionzi inasema tiba ya mionzi inachangia sehemu kubwa ya mionzi inayowakumba watu.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo na UNSCEAR inasema tiba ya mionzi inachukua asilimia 98 ya vyanzo vyote vya mionzi na ni ya pili kwa uchangiaji wa idadi ya mionzi inayowapata watu kote duniani.

UNSCEAR ikiwasilisha ripoti hiyo kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa imesema kiwango kikubwa cha mionzi kina madhara kwa mwili wa binadamu na kinaweza kusababisha kifo,na kutumia mionzi kwa muda mrefu kunaongeza hatari ya maradhi zaidi.

Matokeo ya ripoti hiyo yametokana na takwimu zilizokusanywa kuanzia mwaka 1997 hadi 2007 ambazo zinaonyesha kwamba takribani vipimo bilioni 3.6 vya X-ray hufanyika kila mwaka ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 ikilinganishwa na muongo uliopita.