Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIFIL imejadili usalama na viongozi wa Lebanon

UNIFIL imejadili usalama na viongozi wa Lebanon

Kamanda wa vikosi vya muda vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL Meja jenerali Albero Asarta Cuevas leo amekuwa na mkutano na spika wa bunge na waziri mkuu wa Lebanon mjini Beiruti.

Mkutano wao umejadili masuala ya usalama kusini mwa Lebanon, uchunguzi wa UNIFIL kuhusu tukio la El Adeisse la Agosti 3 na utekelezaji wa azimio namba 1701 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano wao pia Meja jenerali Asarta amesisitiza umuhimu wa wa kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya UNIFIL na majeshi yaliyo na silaha ya Lebanon.

Kuhusu tukio la El Adeisse amesema amepata hakikisho kutoka pande zote kwamba zinataka kuondoa mvutano na kuendelea kufanya kazi na UNIFIL ili kurejesha utulivu katika eneo hilo la mpakani.