Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa

UM umezindua muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa

Umoja wa Mataifa leo umezindua muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa duniani

Vita hivyo vina lengo la kuhamasisha na kuchagiza kuchukua hatua ili kuimarisha ulindaji wa maeneo makame ya dunia ambayo ni makazi ya theluthi moja ya watu wote duniani, wanakabiliwa na tishio kubwa la kiuchumi na mazingira.

Katika ujumbe maalumu wa uzinduzi wa leo ambao kimataifa umefanyika Fortaleza Brazili katika jimbo la Ceara ambalo pia ni nusu jangwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ba Ki-moon amesema wakati tukianza muongo mzima wa vita dhidi ya ukame na jangwa tuongeze juhudi la kulinda ardhi ambayo tunaitegemea katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia na kutuhakikishia uhai wetu.

Kimataifa ukame na jangwa vimeathiri ekari milioni 3.6 na unatishia maisha ya watu zaidi ya bilioni moja katika nchi 100 duniani. Mbali ya uzinduzi wa kimataifa ule wa kanda ya Afrika umefanyika mjini Nairobi kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP na mratibu wa UNEP Kenya Henry Ndede anafafanua kuhusu athari za jangwa Afrika.

(SAUTI YA HENRY NDEDE)