Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aahidi kuchagiza misaada zaidi kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Ban aahidi kuchagiza misaada zaidi kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Mtu mmoja kati ya 10 ameathirika na mafuriko yaliyoikumba Pakistan katika wiki mbili zilizopita. Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anayezuru Pakistan leo Jumapili ameahidi kuchagiza haraka misaada ya jumuiya ya kimataifa kwa watu milioni 20 walioathirika na kuonya kwamba matatizo katika nchi hiyo ya asia hataisha leo.

Katibu Mkuu ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba yuko nchini humo ili kuitolea wito dunia kuongeza juhudi za msaada wao kwa Pakistan.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameahidi kuwasilisha tatizo hilo kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Alhamisi ijayo ili kujaribu kuchagiza msaada wowote unaohitajika kwa watu wa Pakistan. Amewahakikishia watu wan chi hiyo kwamba dunia nzima iko pamoja na watu hao katika kipindi hiki kigumu cha majaribu.

Na ameongeza kuwa ana imani kwamba ujasiri, matumaini na mshikamano wa watu wa Pakistan na serikali yao utasaidia kuyashinda matatizo yote yaliyosababishwa na mafuriko na kuganga yajayo.