Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kuongoza misaada wa waathirika wa maporomoko China

UNICEF kuongoza misaada wa waathirika wa maporomoko China

Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF linafanya mipango ya kusambaza misaada kaskazini magharibi mwa China kuusadia utawala wa nchi hiyo kukabilina na janga na maporomoko ya udongo ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 700.

Hadi sasa takriban watu wengine 1000 hawajulikani walipo huku wengine 45,000 wakiondolewa kutoka mkoa wa Gansu ulioshuhudiwa maporomo makubwa ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa. Maporomoko hayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kuikumba china kwa miongo sita huku juhudi za uokozi zikitatizwa na mvua na udongo unaofunga barabra hasa kwenye maeneo ya milima.

Maafisa wa UNICEF ambao wamekuwa wakifanya kazi na maafisa wa serikali ya China wanasema kuwa wanapamga kutoka misaada kwa akina mama na pia kuwapa chanjo dhidhi ya maradhi watoto wadogo 10,000