Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeonya kuwa tatizo la Pakistani litakuwa la muda mrefu

UNHCR imeonya kuwa tatizo la Pakistani litakuwa la muda mrefu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kwamba matatizo yanayoikabili Pakistan hivi sasa sio tuu ni makubwa bali pia ni yanayoendelea.

Shirika hilo linasema kutaendelea kuwa na uharibifu mkubwa baada ya mito kufurika na maji kuelekea upande wa kusini, na limeongeza kuwa hata mafuriko yakimalizika matatizo hayataisha kutokana na athari za mafuriko hayo ambayo yamewaacha mamilioni bila makazi, njaa na maradhi.

UNHCR imenunu mahema ya dharura 69,000 kuwasaidia waathirika na linawasaidia sio tuu waathirika wa Pakistan bali pia hata wan chi jirani ya Afghanistan. Na linasema hofu yake kwa sasa ni mamilioni ya walioachwa bila makazi Pakistan na ambao hawajafikiwa na msaada wowote.