Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inawasaidia waathirika wa mafuriko nchini Chad

UNHCR inawasaidia waathirika wa mafuriko nchini Chad

Mafuriko yameathiri sehemu kubwa ya Chad tangu katikati ya mwezi Julai kufuatia mvua kubwa kuwahi kunyesha katika kipindi cha miaka 40.

Watu wapato 9000 inasemekana wameathirika na mafuriko hayo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linazisaidia familia zaidi ta 2000 zilizoathirika kwa kugawa vitu mbalimbali vikiwemo mablanketi. Msaada huu unawafikia walengwa kwa mchango mkubwa wa juhudi za kitaifa zinazoendelea kwa utaribu wa serikali ya Chad ambapo mashirika ya umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanashiriki pia. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(CLIP AFRIAN EDWARD UNHCR)

Mvua hizo zimetoa matumaini kwa baadhi ya wakulima lakini katika maeneo mengine mashamba na vijiji vimesambaratishwa kabisa na mafuriko hayo.