Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM imeanza mipango ya kuzuaia moto makambini Haiti

IOM imeanza mipango ya kuzuaia moto makambini Haiti

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza mipango ya kusaidia kuchukua hatua za kupunguza hatari ya moto kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani nchini Haiti.

Hatua hiyo imekuja baada ya moto uliozuka kwenye moja ya kambi mjini Port-au-Prince kukatili maisha ya mtoto mmoja na kuteketeza mahema manne wiki hii. Upepo mkali mara nyingi huvuma kuelekea kwenye makambi hayo ya muda ambayo yana idadi kubwa ya wakimbizi wanaolala kwenye mahema yaliyoezekwa kwa maplastiki.

Wengi wa wakimbizi wanatumia taa za kandili na koroboi ambavyo ni hatari kubwa kwa kuzusha moto. Wakimbizi wa ndani milioni 1.5 hadi sasa hawana makazi nchini Haiti tangu kuzuka kwa tetemeko kubwa la ardhi mwezi Januari mwaka huu, na ajali ya moto ni moja ya hatari kubwa zinazowakabili wakiwa kambini.