Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Hiroshima Ban amesema dunia bila silaha za nyuklia ndio njia pekee ya usalama duniani

Akiwa Hiroshima Ban amesema dunia bila silaha za nyuklia ndio njia pekee ya usalama duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amesema inawezekana kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia.

Ameyasema hayo leo akiwa bega kwa bega na manusura wa shambulio la bomu la atomic la Hiroshima pamoja na maelfu ya watu waliokusanyika katika sherehe za kumbukumbu ya amani ya miaka 65 ya shambulio hilo nchini Japan. Ban amewaambia waliokusanyika kwamba dunia ya amani inaweza kuwa yetu na mbali ya kutoa heshma zake kwa walioathirika na shambulio hilo ana ujumbe maalumu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban Ki-moon ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza kushiriki sherehe za kumbukumbu ya Hiroshima na Nagasaki alikuwa na umri wa mwaka mmoja tuu wakati Marekani ilipodondosha mambomu ya atomic katika miji hiyo miwili Agosti 1945, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200,000, na hadi leo watu wengine zaidi ya 400,000 wamekufa na athari za shambulio hilo.

Ban amesema ikiwa silaha za nyuklia zitaendelea kuwepo basi tishio litakuwepo pia, kama tunataka kuondoa tishio basi tutokomeze silaha hizo ndio maana amesema 2008 alipendekeza vipengele vitano vya upokonyaji na kutozalisha nyuklia, na kwa sasa anasema hatua zimepigwa.

(SAUTI BAN -2)

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano katika ujumbe maalumu wa kuazimisha kumbukumbu hii amesema anajidhatiti kuongeza mara mbili juhudi za kuelekea kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

Amano ameongeza kuwa majina Hiroshima na Nagasaki yameingia katika historia ya athari za nyuklia. Hivyo tunastahili kuwalipa kwa juhudi zetu ,za kuhakikisha kwa kila njia hatutoshuhudia Hiroshima au Nagasaki nyingine.