Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNOCI imesema inazingatia tarehe ya uchaguzi iliyotangazwa Ivory Coast

UNOCI imesema inazingatia tarehe ya uchaguzi iliyotangazwa Ivory Coast

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI umesema unazingatia tarehe mpya ya uchaguzi wa Rais ambayo imetangazwa jana na serikali.

Serikali imethibitisha kwamba sasa uchaguzi baada ya kucheleweshwa kwa muda mrefu utafanyika tarehe 31 Oktoba kufuatia pendekezo la tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo Awali uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi ambayo iligawika mapande mawili na vita vya wenyewe kwa wenyewe 2002.

Vita hivyo  vililifanya eneo la Kaskazini kudhibitiwa na waasi na la kusini na serikali, ulikuwa ufanyike 2005 lakini umekuwa ukiahirishwa kutokana na sababu mbalimbali. UNOCI imewataka wadau wote kuweka ratiba muafaka itakashoghulikia mipango na changamoto zingine kabla ya siku ya uchaguzi, na hatua muhimu ni kuchapisha orodha ya mwisho ya wapiga kura.