Matatizo ya kiuchumi yamesababisha kuporomoka kwa mavuno ya mbao:UNECE

Matatizo ya kiuchumi yamesababisha kuporomoka kwa mavuno ya mbao:UNECE

Ripoti mpya iliyotolewa leo inasema matumizi ya bidhaa za mbao na vifaa vitokanavyo na karatasi yamepungua kwa asilimia 11 mwaka 2009 nchini Marekani, Ulaya na nchi za jumuiya ya madola.

Ripoti hiyo ya mwaka ya tathimini ya soko la bidhaa za misitu kwa mwaka 2009-2010 iliyochapishwa na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa bara Ulaya UNECE kwa ushirikiano na shirika la chakula na kilimo FAO inasema kiwango hicho cha kuporomoka ni kikumbwa sana tangu kuzuka kwa matatizo ya mafuta miaka ya 1970.

Ripoti hiyo inasema sababu kubwa ya kuporomoka huko ni athari za za mwaka 2008-2009 zilizoikumba sekta hiyo ambazo zimeshuhudia soko la nyumbalikianguka nchini Marekani.