Skip to main content

UM umeingilia kati kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

UM umeingilia kati kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Umoja wa Mataifa umezitaka Israel na Lebanon kujizuia kuendeleza mvutano baada ya majibizano ya risasi jana kwenye eneo linalozigawa nchi hizo mbili la msitari wa bluu.

Wanajeshi wa kulinda amani kutoka kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL wako katika eneo la El Adeisse na wanajaribu kutuliza hali ya mambo na kuzuia uwezekano wa vifo. Andrea Tenenti ni naibu msemaji wa UNIFIL

(CLIP ANDREA TENENTI)

Duru za habari zinasema wanajeshi watatu wa Lebanon na mwandishi habari mmoja waliuawa katika majibishano hayo ya risasi. Kuheshimu msitari wa bluu ni moja ya masharti ya azimio 1701 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilimaliza vita vilivyozuka 2006 kati ya Israel na kundi la Hizbollah la Lebanon.