Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya waathirika wa mafuriko Pakistan wanahitaji malazi :UNHCR

Maelfu ya waathirika wa mafuriko Pakistan wanahitaji malazi :UNHCR

Wakati huohuo shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR imeongeza juhudi za kuwapatia malazi maelfu ya watu walioathirika na mafuriko nchini Pakistan.

Shirika hilo linasema hadi sasa wameshagawa mahema 100,000 na vifaa vingine vya malazi katika maeneo ya Baluchistan na Pakhtunkhwa majimbo mawili yaliyoathirika sana. UNHCR inasema wanashirikiana na serikali ili kuwafikia watu 250,000 ambao wanahitaji msaada wa haraka wa malazi na vitu vingine visivyo chakula.

Kamishna mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres amesema Wapakistan katika eneo lililoathirika kwa muda wamekuwa wakiwahifadhi zaidi wa wakimbizi milioni moja wa Afghanistan na sasa ni wakati wa jumuiya ya kimataifa kuonyesha mshikamano na kuwasaidia.