UM wahofia Nepal na wapiganaji wa Kimao kuanza kusajili watu wapya

UM wahofia Nepal na wapiganaji wa Kimao kuanza kusajili watu wapya

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Nepal leo umeelezea hofu yake kuhusu taarifa kwamba jeshi la serikali na jeshi la wapiganaji wa Kimao wana mpango wa kuanza kusajili watu wapya jambo ambalo litakiuka makubaliano ya amani ya 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mpango huo wa Umoja wa Mataifa UNMIN unasema kusajili watu wapya kwa upande wowote ule pia kutakiuka makubaliano ya silaha yaliyotiwa saini na pande hizo mbili . UNMIN iliundwa kusaidia mchakato wa Amani nchini Nepal na jukumu lake ni pamoja na kuangalia matumizi ya silaha kwa wanajeshi wa pande zote na pia kusaidia kusimamia mkataba wa kusitisha vita usikiukwe.

UNMIN imekumbusha kwamba kusajili watu wapya kwa upande wowote hata kama ni kuziba pengo la walioondoka hakuruhusiwi isipokuwa tuu kama pande zote zimeafiki.