Zaidi ya watu 250,000 wametia sahihi kampeni ya FAO kutokomeza njaa

Zaidi ya watu 250,000 wametia sahihi kampeni ya FAO kutokomeza njaa

Zaidi ya watu 250,000 wameshatia sahihi kampeni ya shirika la chakula na kilimo FAO ya kupinga njaa kwenye wavuti wa shirika hilo wa 1billionhungry.org.

Kampeni hiyo ya dunia nzima ni ya kuzitaka serikali kulipa kipaumbele suala la kutokomeza njaa. Mkurugenzi wa FAO Jacques Diouf anasema hatua zimepigwa na zinaendelea vizuri, lengo ni kupata sahihi milioni moja ifikapo mwishoni mwa Novemba. Ametoa wito kwa kila mtu kutia sahihi kampeni hiyo kwenye wavuti ili kuonyesha mshikamano wa kutokomeza njaa.

Ameongeza kuwa wataendelea kuzitia shinikizo serikali hadi lengo la kumaliza njaa litakapotimia. Moja ya vitu wanavyotumia kuchagiza kampeni hiyo ni video iliyotengenezwa na mcheza filamu wa uingereza Jeremy Irons.