Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya misaada ya UM yameongeza juhudi kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Mashirika ya misaada ya UM yameongeza juhudi kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Wafanyakazi wa misaada bado wanahangaika kuwafikiwa zaidi ya watu 27,000 waliokwamba kutokana na mafuriko nchini Pakistan.

Wafanyakazi hao wanasema uharibifu mkubwa kwenye miundombinu kama barabara na kubomoka kwa madaraja kumefanya iwe vigumu kufikia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mafuriko yanayoendelea kutokana na mvua ambazo bado zinanyesha.

Idadi ya waliokufa sasa imefikia zaidi ya 1400 na inatarajiwa kuongezeka. Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF aliyezuru baadhi ya maeneo yaliyoathirika Martin Mogwanja anasema nyumba nyingi zimegeuka tope, mazao yamesombwa na maji na miti mingi imeangua. Hali ni mbaya

(SAUTI YA MOGWANJA )

Shirika la afya duniani WHO na washirika wake linaisaidia serikali ya Pakistan kwa kupeleka madawa na vifaa vingine vya afya kwa ajili ya kuwatibu zaidi ya watu 200,000 katika maeneo yaliyoathirika, kama anavyoeleza Fadela Chaib kutoka WHO

(SAUTI YA FADELA CHAIB)

Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema linaendelea kugawa chakula cha dharura kwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo ya Peshawar, Mardan, Charsadda na Nowshera, na linakadiria kwamba watu milioni 1.8 watahitaji msaada wa dharura.