Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola 200,000 zipo tayari kwa mshindi wa tuzo ya Sakakawa 2011:UNEP

Dola 200,000 zipo tayari kwa mshindi wa tuzo ya Sakakawa 2011:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na mfuko wa The Nippon leo wamezindua rasmi mjini Nairobi shindalo la tuzo ya UNEP ya Sasakawa kwa mwaka 2011.

Tuzo hiyo inamtafuta mshindi wa mradi wenye ubunifu mkubwa wa kulinda mazingira kutoka nchi zinazoendelea, na zawadi nono ya dola 200,000 itatolewa kwa mshindi. Tuzo ya Sasakawa hutokewa kila mwaka kwa mashirika ya mashinani ambayo ymetoa mchango mkubwa wa kulinda na kuboresha mazingira na kuleta maendeleo katika jamii. Mada kuu katika shindalo la mwaka huu ni "misitu kwa ajili ya watu, misitu kwa maendeleo yanayojali mazingira" kwa kuunga mkono mwaka wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa misitu ambao ni 2011.

Mambo ambayo majaji watayapa kiupaumbele mwaka huu ni kuchagiza kulinda mazingira na kuendeleza misitu, mchango katika kupunguza gesi ya cabon inayochangiwa na ukataji miti, kulinda misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kusaidia maendeleo katika jamii zinazotegemea misitu na kulinda bayoanuai. Tuzo ya UNEP ya Sasakawa ilianzishwa ili kuchagiza ubunifu na utafiti wa suluhisho la changamoto za mazingira kwa kutoa msaada wa fedha kwa mshindi.