Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inachukua mipango mipya kukabiliana na maradhi ya mifugo

FAO inachukua mipango mipya kukabiliana na maradhi ya mifugo

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema hatua imara za kuzuia na kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mifugo zinaweza kusaidia kuokoa fedha nyingi kwa serikali.

FAO imeyasema hayo leo ikitangaza mipango mipya ambayo ni imara zaidi ya kubaini na kukabiliana na magonjwa ya mifugo. FAO inasema kutokana na uzoefu wake imeona ni bora kuwa na mipango ambayo ina lengo la kuchukua hatua za haraka kukabiliana na milipuko ya magonjwa, kutekeleza mipango ya kukinga, mipango ya tahadhari na kukabiliana na athari.

Mipango hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO na shirika la kimataifa la afya ya wanyama. FAO inawaomba wahisani kuwekeza katika mipango hiyo ya miaka mitano.