Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi kwa 2010 umemalizika Vienna Austria

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi kwa 2010 umemalizika Vienna Austria

Mkutano wa 18 wa kimataifa wa ukimwi mwaka 2010 umemalizika leo mjini Vienna nchini Austria.

Mkutano huo ulioanza Julai 18 umehudhuriwa na wajumbe na wawakilishi 20,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kauli mbiu ya mkutano ilikuwa "ni hapa na ni sasa hivi" ikitoa msisitizo wa hali mbaya ya uhusiano uliopo baina ya ugonjwa wa ukimwi na binadamu. Mada kadhaa zimejadiliwa katika mkutano huo ikiwemo uhusiano baina ya unyanyapaa na ongezeko la kusambaa kwa ukimwi, hali ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi makazini, fursa ya watu zaidi kuweza kupata dawa na ukimwi katika magereza.

Manfred Nowark ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya utesaji anasema hali ya ukimwi katika magereza nchini nyingi duniani imefurutu ada.

(SAUTI YA MANFRED NOWARK)