Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umekaribisha hatua ya Eritrea na Djibouti kumaliza mzozo wa mpaka

UM umekaribisha hatua ya Eritrea na Djibouti kumaliza mzozo wa mpaka

Umoja wa Mataifa leo umekaribisha hatua ya Eritrea na Djibouti ya kutatua mzozo wao wa mpaka kupitia upatanishi wa Qatar.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada wa kiufundi kama unahitajika ili kukamilisha muafaka huo. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kisiasa B.Lynn Pascoe ameliambia baraza la usalama kwamba waziri mkuu wa Qatar Sheikh Hamad bin Jabr Al-Thani alimuandikia Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon kumfahamisha kwamba vikosi vya Eritrea vimeondoka kutoka eneo la mpaka linalozozaniwa la Ras Doumiera na kisiwa cha Doumiera na na wanajeshi wa Qatar wamepelekwa eneo hilo kwa uangalizi wakisubiri hatua ya mwisho ya maafikiano.

Hatua hiyo inafuatia kutia sahihi makubaliano baina ya Eritrea na Djibouti tarehe 6 Juni mwaka huu chini ya upatanishi wa serikali ya Qatar ambapo nchi hizo majirani waliamua kumaliza mzozo wao kwa njia ya majadiliano.

Machi 2008 Eritrea ilipeleka vikosi na vifaa vya kijeshi katika maeneo hayo mawili ambayo ni mpaka baina ya Eritrea na Djibouti.