Skip to main content

Katika mkutano mkubwa Kabul UM waahidi msaada wa muda mrefu kwa Afghanistan

Katika mkutano mkubwa Kabul UM waahidi msaada wa muda mrefu kwa Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan mjini Kabul amesema wakati jumuiya ya kimataifa wakati mwingine haikutilia maanani sana historian na utamaduni wa Afghanistan, mchakato wa Kabul ulioanza leo una nia ya kujitahidi zaidi kwa ajili ya taifa hilo.

Ban amesema serikali ya Kabul imechukua jukumu la kuatayarisha mipango ambayo jumuiya ya kimataifa itaiunga mkono. Mipango hiyo ina lengo la kuhakikisha inazaa matunda kwa watu wa Afghanistan bila kuchelewa, kuwa na utawala imara wa kidemokrasia na kuwahakikishia haki na utawala wa sheria watu wa nchi hiyo.

Pia Ban amewatole wito watu wa taiafa hilo kuungana ili kupata amani kwa njia ya maridhiano na kuweza  kujenga hatma yao ya kiuchumi,maendeleo na kuheshimu uhuru wao.

(SAUTI BAN KI-MOON)