Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya kihalifu vya vikosi vya usalama vinatishia amani Kyrgystan

Vitendo vya kihalifu vya vikosi vya usalama vinatishia amani Kyrgystan

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema ana taarifa kwamba vikosi vya usalama Kusini mwa Kyrgystan vinahusika na vitendo vya mara kwa mara vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Vitendo hivyo ni pamoja na kuwaweka watu mahabusu kiholela, utesaji na kuwanyanyasa watu. Bi Pillay amesema vitendo hivyo vinatishia amani ambyo yatari ina utata na suala la kurejesha tena utawala wa sheria wiki sita baada ya machafuko yaliyolitikisa taifa hilo la Asia ya Kati.

Ameongeza kuwa idadi kubwa ya vijana wa kiume wengi wakiwa wa kbila la Uzbek wamekuwa wakishikiliwa kiholela katika njia mbayo sio tuu inaonyesha ubaguzi dhidi ya watu hao bali pia inakiuka sheria za kimataifa kwa wote Wauzbek na Wakyrgy.Rupert Colville ni msemahi wa haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE))