Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Karzai amesema Afghanistan itakuwa tayari kujilinda ifikapo 2014

Rais Karzai amesema Afghanistan itakuwa tayari kujilinda ifikapo 2014

Naye Rais Hamid Karzai wa Afghanistn akizunguma kwenye mkutano huo wa kimataifa mjini Kabul amesema anaamini majeshi ya ulinzi na usalama ya nchi yake yatakuwa tayari kuchukua jukumu la usalama wa nchi hiyo ifikapo 2014.

Muda huo wa miaka mine umeidhinishwa katika azimio lilillotolewa na washiriki wa mkutano huo ambao ni pamoja na mataifa ya magharibi wachangiaji wa vikosi vya muungano vinavyokabiliana na wanamgambo wa Taliban nchini humo.

Hali ya usalama hivi sasa ni mbaya na mfano dhahiri umejitokeza leo baada ya ndege ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ilipolazimika kuondokea kwenye kiwanja kingine badala ya Kabul kutokana na shambulio la maroketi. Karzai amesema amefurahi kuona jumuiya ya kimataifa iko tayari kuendelea kuisaidia nchi yake.

(SAUTI KARZAI AFGHAN)