Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wa Darfur na UM kutia saihini mkataba wa kuwalinda watoto

Waasi wa Darfur na UM kutia saihini mkataba wa kuwalinda watoto

Waasi wa jimbo la Darfur Sudan na Umoja wa Mataifa wiki hii wanatia sahii mkataba wa kuwalinda watoto.

Taarifa hii imetolewa leo na kundi binafsi la uopatanishi na inasema hatua hii ina lengo la kusitisha utumiaji wa watoto jeshini. Kituo cha mazungumzo ya kijamii kimesema kundi la Justice and Equality Movement JEM na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF watatia sahihi makubaliano mjini Geneva siku ya Jumatano ijayo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamepata ushahidi kwamba JEM, waasi wengine na makundi yanayoiunga mkono serikali wamekuwa wakiwafunza na kuwatumia wanajeshi watoto katika vita baada ya kuzuka machafuko ya 2003 wakati wanamgambo ambao sio Waarabu walipopambana na serikali wakitafuta kujitawala.