Uwekezaji katika hali ya hewa ni muhimu kwa siku za usoni:Ban

Uwekezaji katika hali ya hewa ni muhimu kwa siku za usoni:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwekeza kifedha katika hali ya hewa ni uwekezaji salama, safi na wa matumaini mazuri kwetu sote katika siku za baadaye.

Ban ameyasema hayo baada ya mkutano na mwenyekiti mwenza wa kundi la ngazi za juu la ushauri kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Ban amesema viongozi wa dunia lazima watimize ahadi zao za msaada kwa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

(SAUTI YA BAN )

Amesisitiza kwamba ni muhimu kujenga hamasa ya majadiliano ya kimataifa kuhusu suala hili, kwani mabadiliko ya hali ya hewa sio jambo linalokwisha.