Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo mpya wa matibabu ya HIV waweza kuokoa maisha ya watu milioni 10:UNAIDS

Mtazamo mpya wa matibabu ya HIV waweza kuokoa maisha ya watu milioni 10:UNAIDS

Ripoti mpya ya mtazamo iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi UNAIDS inasema vifo vingi na maambukizi mapya vinaweza kuepukwa.

Ripoti hiyo inasema vijana wanaongoza katika mapinduzi ya kuzuia maambukizi huku nchi 15 kati ya zilizoathirika sana na ukimwi zikiarifu kushuka kwa asilimia 25 ya maambukizi kwa vijana, ambao sasa wanakumbatia ngono salama.

Ripoti hiyo ya UNAIDS inaainisha matibabu ya HIV yaitwayo Treatment 2.0 ambayo yanaweza kupunguza idadi kubwa ya vifo na maambukizi mapya. Michel Sidibe ni mkurugenzi mkuu wa UNAIDS

(SAUTI YA MICHEL SIDIBE)