Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wanatathimini kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake

Wataalamu wa UM wanatathimini kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake

Mkutano wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake unaendele leo hapa New York.

Mkutano huo ulioanza jana unatathimini hali ya wanawake katika nchi nane ikiwemo Papua New Guinea ambayo inatathiminiwa kwa mara ya kwanza na India itakayopewa mtazamo wa kipekee. Masuala ya ukatili dhidi ya wanawake, ushiriki wa kisiasa, ubaguzi wa sheria za familia, kukomesha dosari za kijinsia na kuzuia usafirishaji haramu wa wanawke ni baadhi ya mambo yatakayochambuliwa na kamati hiyo, iliyo na jukumu la kuhakikisha kwamba serikali zote duniani zinatokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake.

Katika siku 19 za mkutano huo kamati ya kukomesha ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW itatathimini hali ya wanawake nchini Argentina, Fiji, Urusi, Australia, Papua New Guinea, India na Albania.