Skip to main content

WHO inaisaidia Nigeria kupambana na ugonjwa wa sumu ya risasi

WHO inaisaidia Nigeria kupambana na ugonjwa wa sumu ya risasi

Shirika la afya duniani WHO linashirikiana na serikali ya Nigeria kudhidibi mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na sumu itokanayo na risasi kaskazini mwa nchi hiyo.

Ugonjwa huo umeelezwa kuwa ni matokeo ya uchekechaji wa chuma cha pua kwenye mgodi wa dhahabu. Mapema mwaka huu shirika lisilo la kiserikali la madaktari wasio na mipaka Medecins sans Frontieres (MSF) waliijulisha wizara ya afya katika jimbo la Zamfara juu ya ongezeko la vifo na maradhi kwa watoto kwenye vijiji vya Bukkuyum na Anka.

WHO ilijiunga na jopo la uchunguzi wa kimataifa ambalo limethibitisha kwamba zaidi ya watoto 100 katika eneo hilo wanaumwa ugonjwa utokanao na sumu ya risasi. WHO imepeleka wataalamu wa afya ili kufanya uchunguzi zaidi kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo na pia kuzuia usitokee tena siku za usoni.