Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano baina ya Sudan na Chad waendelea kuimarika:Gambari

Uhusiano baina ya Sudan na Chad waendelea kuimarika:Gambari

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ibrahimu Gambari amesema uhusiano baina ya Sudan na Chad unaendelea kuimarika.

Aklizungumza mjini El-Fasher kwenye jimbo la Darfur amesema kuwajibika kwa nchi hizo mbili kumesaidia kuleta hali ya utulivu katika mpaka wao.

Gambari ameongeza kuwa kurejea katika hali ya kawaida kwa uhusiano huo kumekuwa na athari nzuri katika suala zima la migogoro baiana ya Chad na Sudan.

(SAUTI YA  GAMBARI)