Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID inaendesha mafunzo kuwaokoa wanawake dhidi ya ukatili

UNAMID inaendesha mafunzo kuwaokoa wanawake dhidi ya ukatili

Duru mbalimbali kwenye jimbo la Darfur Sudan zinasema visa vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ni suala lililomea mizizi na hususan karibu na makambi ya wakimbizi wa ndani.

Katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo jeshi la polisi la Sudan GOS pamoja na polisi wa SLA wajulikanao kama Minni Minawi wanapatiwa mafunzo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na kukabiliana na kesi za ukatili dhidi ya wanawake.

Mafunzo hayo yanatolewa na ofisi ya jeli la kulinda amani la Umoja wa Mataifa na ule wa Afrika Darfur UNAMID, kitengo cha utawala wa sheria, haki za binadamu na jinsia.