Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuyasifu mataifa ya Caribbean kwa juhudi zao za kusaidi nchi ya Haiti

Ban kuyasifu mataifa ya Caribbean kwa juhudi zao za kusaidi nchi ya Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesifu mataifa ya eneo la Caribbean kwa juhudi zao za kusaidia nchi ya Haiti kufuatia tetemeko kubwa la ardhi iliyokumba nchi hiyo mwezi wa Januari mwaka huu, na kuhimiza mataifa hayo kuzidi kusaidia kwani taifa hilo litahitaji usaidizi wa kimataifa.

Ban ameyaambia mataifa hayo kuwa kuzidi kushiriki kwenu ni muhimu kwa juhudi ya muda mrefu ya kuisaidia nchi hiyo akiongeza kuwa amesema amefurahi kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuhutubia mkutano wa CARICOM.

Alisema atazidi kuipa Haiti kipao mbele katika ajenda yake katika Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa uchaguzi wa Novemba nchini humo utakuwa ni muhimu kwa hali ya baadae ya demokrasi nchini humo