Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa haraka wa dawa unahitajika nchini Kyrgystan:OCHA

Msaada wa haraka wa dawa unahitajika nchini Kyrgystan:OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuratibu masuala ya kibinadamu OCHa imesema kuna haja ya haraka ya kupatikana dawa nchini Kyrgystan.

Akizungumza mjini Geneva msemaji wa OCHA Elizabeth Byers amesema, kwa mujibu wa serikali ya Kyrgystan watu wote wanaohitaji msaada wa madawa isipokuwa 395 wameondoka Uzbekistan.

Ameongeza kuwa takribani asilimia 96 ya wakimbizi wote wamerejea nchini Kyrgystan. OCHA inasema juhudi za kimataifa za misaada ya kibinadamu sasa zinawalenga zaidi wale waliorejea nyumbani ambao wengi nyumba zao ziliharibiwa na machafuko.