Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inawasaidia zaidi ya wakimbizi wa ndani 375,000 Kyrgystan

UNHCR inawasaidia zaidi ya wakimbizi wa ndani 375,000 Kyrgystan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UHNCR linasema hali kusini mwa Kyrgystan imesalia kuwa ya utulivu.

Hali ya kuwafikia wahitaji wa misaada katika maeneo ya Osh, Jalalabad na vijijini katika eneo hilo inaimarika. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema kuna uharibiru mkubwa kusini mwa nchi hiyo, huku asilimia 95 ya nyumba zimeharibika vibaya katika mji wa Osh. Inakadiriwa kuwa watu 375,000 wameachwa bila makao ikiwa ni pamoja na wanaorejea kutoka Uzbekistan (SAUTI YA  ADRIAN UNHCR)

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa wakimbizi Antonio Guterres kesho anaanza ziara ya siku mbili Kyrgystan kutathimini hali halisi ya wakimbizi wa ndani pia kukutana na Rais na viongozi wengine wa serikali ya nchi hiyo. Umoja wa Mataifa uliomba msaada wa dola milioni 73 ili kutoa msaada wa dharura Kyrgystan na hadi sasa dola milioni 11.5 ndio zilizopatikana ambazo ni asimilia 16 ya fedha zinazohitajika.