Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano katika ardhi unawanufaisha wawekezaji na wakulima:FAO

Ushirikiano katika ardhi unawanufaisha wawekezaji na wakulima:FAO

Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo inaonyesha kwamba uwekezaji katika kilimo kwenye nchi zinazoendelea unaweza kutumika kama mbadala wa umilikaji ardhi kubwa.

Ripoti hiyo inaainisha njia mbalimbali za kufanya biashara ambazo zitaleta faida kwa wakulima wadogo wadogo na kulinda haki zao za ardhi, wakati huohuo zikihakikisha faida kwa makampuni yanayowekeza. Ripoti hiyo imetolewa leo na taasisi ya kimataifa ya maendeleo na mazingira (IIED) na iliagizwa na shirika la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la Uswis kwa ajili na maendeleo na ushirikiano SDC.

Ripoti hiyo inasema ingawa uwekezaji katika kilimo unaweza kuzinufaisha nchi zinazoendelea, lakini inaonya kuwa kuwekeza kunaambatana na hatari kwani wazawa wanaweza kupoteza haki na rasilimali waliyoimiliki kwa vizazi vingi.