Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa amani umekuwa kitu tofauti na uzoefu wa mafanikio:Ban

Ulinzi wa amani umekuwa kitu tofauti na uzoefu wa mafanikio:Ban

Mafanikio ya ulinzi wa amani limekuwa ni jukumu letu sote. Hivyo ndivyo alivyosema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika taarifa yake kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukijadili hatma ya vikosi vya kulinda amani.

Katibu Mkuu ametaka kuwepo ushirikiano na wale wanaoongoza opeeresheni za kulinda amani, wanaochangia na wanaosimamia shughuli katika maeneo husika. Amesema washirika wa kikanda na wale ndani wana faida kubwa, taasisi za kimataifa za fedha na wadau wengine wa maendeleo wana mchango mkubwa wa kutoa, na serikali husika lazima iwe mfano. Na kwa nchi wanachama lazima waunde malengo ambayo yako bayana na yatakayoweza kufikiwa kutokana na rasilimali na utalaamu uliopo.

Ban ameongeza kuwa familia yote ya Umoja wa Mataifa lazima ishiriki. Shughuli za kulinda amani zitaendelea kuja na matatizo mbalimbali kama mipango ya kuondoka na matakwa ya nchi husika. Lazima pia tufikirie kwa mapana na marefu jinsi gani ya kuimarisha upatanishi, kuzuia migogoro na ujenzi wa amani baada ya vita, jinsi gani ya kudumisha haki duniani na jinsi gani ya kushugulikia wachochezi wa kiuchumi wa vita.

Katibu Mkuu amesema ulinzi wa amani imekuwa ni suala tofauti na uzoefu wa mafanikio, lakini kuna haja ya kuondoa zana zetu, amesema hilo litawezekana tuu kwa nchi wanachama kuendelea kujihusisha, sio tuu kutoa vikosi bali pia mchango wa fedha na wa kisiasa.