Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa polisi wa UM anatumia ujuzi wake kuwasaidia wengine nchini Liberia

Afisa wa polisi wa UM anatumia ujuzi wake kuwasaidia wengine nchini Liberia

Afisa wa polisi anayefanya kazi na mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia anatumia ujuzi wake kuwapa sauti sio tuu wanawake walioathirika na kubakwa bali pia anawasaidia viziwi wan chi hiyo.

Akizungumza na Umoja wa Mataifa bi Malambo anasema katika tukio hilo hakuna afisa yoyote wa polisi kwenye kituo chao angeweka kuchukua maelezo ya mwanamke huyo kiziwi hivyo alikuwa msaada mkubwa kwa mwanamke huyo kuelewa na kuweza kumsaidia.

Bi Malambo alipata mafunzo ya lugha ya ishara katika nchi anakotoka ya Zambia na imekuwa ni msaada kwa wanaawake wengi wenye matatizo ya kusikia nchini Liberia.