UNHCR imetangaza hatua kubwa iliyopiga kuwapatia makazi wakimbizi wa Iraq

UNHCR imetangaza hatua kubwa iliyopiga kuwapatia makazi wakimbizi wa Iraq

Umoja wa Mataifa leo umetangaza kwamba wakimbizi laki moja wa Iraq wamepatiwa makazi kutoka mashariki ya Kati hadi nchi ya tatu tangu mwaka 2007 jambo ambalo ni hatua kubwa kwa idadi hiyo ya wakimbizi.

Akiwa ziarani nchini Syria kamishna mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres amesema hayo ni mafanikio makubwa .

Syria inahifadhi wakimbizi takriban milioni moja wa Iraq. Bwana Guterres amesema wengi wa wakimbizi wa Iraq watakuwa njia panda endapo serikali hazitafungua milango kuwapa makazi.

Bwana Guterres yuko Syria kwa ajili ya kuadhimisha rasmi kimataifa siku ya wakimbizi duniani Juni 20 ambayo inaadhimishwa nchini humo kwa mara ya kwanza na pia ni mara ya kwanza kwa eneo zima la mashariki ya Kati.