Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa kimataifa umesitisha msaada kwa Zambia kutokana na ufisadi

Mfuko wa kimataifa umesitisha msaada kwa Zambia kutokana na ufisadi

Mfuko wa kimataifa kwa ajili ya ukimwi, kifua kikuu na malaria umesitisha msaada wake kwa wizara ya afya ya Zambia ikihofia kuwepo na ufisadi.

Andrew Hirst, msemaji wa mfuko huo amesema kiasi cha fedha kilichositishwa kupelekwa ni dola milioni 137. (SAUTI YA  HIRST)

Bwana Hirst anaeleza kwamba mfuko huo umechukua hatua za kutoa huduma za kuokoa maisha kwa Wazambia kama kugawa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa ukiwmi, vyandarua vyenye dawa, na dawa za kifua kikuu.

Athari pekee ya kusitisha msaada ni kushindwa kuharakisha mipango iliyokuwepo. Lakini ameongeza kuwa UNDP itachukua jukumu la fedha zilizozuiliwa kutoka wizara ya afya ambazo zitasaidia kuanza tena kwa miradi hiyo.