Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa fedha utaathiri usambazaji wa misaada Afrika Magharibi

Ukosefu wa fedha utaathiri usambazaji wa misaada Afrika Magharibi

Ukosefu wa fedha umelilazimu shirika la misaada ya chakula la Umoja wa Mataifa kusitisha ndege za misaada ya kibinafdamu kwenda katika nchi tatu za Afrika ya magharibi kuanzia leo.

Shirika hilo ambalo ni la mpango wa chakula duniani WFP ambalo linasimamia huduma za ndege za misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UNHAS limesema ndege kwenda Guinea, Sierra Leone na Liberia zitasitishwa kwa sababu shirika hilo limeshindwa kukusanya dola milioni 2.5 zinazotakiwa ili kuendelea na operesheni hadi mwisho wa mwaka huu.

UNHAS imekuwa ikitoa msaada wa usafiri kwa abiria 500 kila mwezi ambao ni watu wanaofanya na mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa wahisani na waandishi wa habari.

Na kwa mujibu wa msemaji wa WFP Emilia Casella msaada huo umekuwa ukiwanufaisha watu laki mbili na nusu kuwafikisha maeno ambayo hayafikiki kwa barabara katika nchi hizo tatu, na pia usafiri huo ulikuwa muhimu kwa masuala ya usalama na kuokoa muda.