Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha unatishia vita vya kimataifa dhidi ya ukimwi:Ban

Upungufu wa fedha unatishia vita vya kimataifa dhidi ya ukimwi:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kwamba Jumuiya ya kimataifa iko katika hatari ya kupoteza vita dhidi ya ukwimi endapo fedha za kufadhili miradi mbalimbali hazitopatikana.

Miradi hiyo ni ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, kuwasaidia waathirika kuishi vizuri hususani barani Afrika.Amesema ferdha hizo ni lazima ziongezwe na zisikosekane. Ban katika waraka aliouandika na kuchapishwa na jarida la Austin Ameriacan-statesman amesema katika vita vyetu vya kimataifa dhidi ya ukimwi ,jumuiya ya kimataifa iko katika hatihati ya kupoteza ushindi.

Amesema fungu la fedha linakauka na baadhi ya wahisani wametishia kupunguza msaada wao kutokana na matatizo ya mdororo wa uchumi, hali ambayo itawaacha mamilioni ya watu wanaoishi na virusi vya HIV kuwa njia panda. Wahisani wengine wameelekeza msaada wao katika magonjwa mengine wanayoona ni nafuu kuyatibu na kuyadhibiti. Ameongeza kuwa wakati ambao tunatakiwa kuchochea juhudi za kufikia malengo ya kupambana na ukimwi, badala yake tunarejea nyuma.

Msaada wa nje umeisaidia Uganda kuongeza idadi ya watu wenye virusi vya HIV wanaopata dawa za kurefusha maisha kutoka 10,000 muongo mmoja uliopita na kufikia 200,000 hivi sasa. Barani afrika inakadiriwa kuwa watu milioni saba ambao wangekuwa wanapata dawa za kurefusha maisha hawapati. Duniani kote watu milioni 10 hawapati dawa hizo.