Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imewasili na misaada ya dharura kuwasaidia wakimbizi Uzbekistan

UNHCR imewasili na misaada ya dharura kuwasaidia wakimbizi Uzbekistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema ndege ya kwanza kati ya mbili zilizosheheni misaada kwa ajili ya maelfu ya wanaokimbia machafuko imewasili Uzbekstan.

Ndege hizo mbili ambazo zimebeba mahema 800, plastiki za kuezekekea , mablanketi na matandiko, ili kukidhi mahitaji ya maelfu ya wakimbizi kutoka kusini mwa Kyrgystan wanaotoroka machafuko mjini Osh. Kwa mujibu wa serikali ya Uzbekistan zaidi ya wakimbizi 75,000 wametafuta hifadhi nchini humo tangu Ijumaa iliyopita.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa wakimbizi Antonio Guterres amekaribisha kuwasili kwa msaada huo na kusema UNHCR inashukuru ushirikiano inaoupata kutoka serikali ya Uzbek kufanikisha kufikisha kwa walengwa msaada huo. Neal Walker ni mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Kyrgystan

(SAUTI YA WALKER )