Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM ataka hatua kali dhidi ya wanaowaingiza watoto jeshini

Mwakilishi wa UM ataka hatua kali dhidi ya wanaowaingiza watoto jeshini

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa leo wamelitaka baraza la usalama kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wa makundi ya waasi na majeshi yanayowaingiza watoto jeshini.

Hatua walizopendekeza ni pamoja na kuzuia mali zao ,vikwazo vya silaha na vikwazo vya usafiri. Na hatua hii iwakumbe sio tuu kwa kuwaingiza watoto jeshini bali hata wanaowadhalilisha kimapenzi, kuwalawiti,kuwatumikisha na kuwauwa wakati wa vita. Mwezi mmoja baada ya Umoja wa Mataifa ya kuwabaini wapiganaji ambao wanaendelea kukiuka haki za watoto katika migogoro, baraza limeombwa kuhakikisha wahalifu hao wanachukuliwa hatua kwa vitendo vyao.

Radhika Coomarwaswamy mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika migogoro ya kutumia silaha amewaambia waandishi wajumbe 15 wa baraza hilo kwamba zoezi la kuwataja na kuwaaibisha ,pamoja na uwezekano wa vikwazo dhidi ya wanaoendelea kunyanyasa watoto, kumesaidia kushawishi baadhi ya wahusika kuacha tabia hiyo na kutawafanya wengine pia kutofanya vitendo hivyo siku za usoni.

(SAUTI YA  COOMARASWAMY)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya Mai kuhusu suala hilo alitaja majeshi na makundi 16 ya wanamgambo Afrika, Asia na Amerika ya Kusini ambaye yaliwaingiza au kutumia wanajeshi watoto katika miaka mitano iliyopita. Bi Coomaraswamy amesema kwamba wengi wa wahusika sio wakuu wa nchi hivyo ambao wanahitaji kujiunga na mpango huu wa Umoja wa Mataifa ili majina yao yaondolewe. Amezitaka serikali kuidhinisha mchakato huu kwa maslahi ya watoto.