Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Kenya imeagiza uchunguzi baada ya watu sita kuuawa katika milipuko

Serikali ya Kenya imeagiza uchunguzi baada ya watu sita kuuawa katika milipuko

Serikali nchini Kenya imeagiza kufanyika uchunguzi kufuatia milipuko miwili ya mabomu iliyoua watu sita na kujeruhi zaidi ya 100 mjini Nairobi.

Shambulio hilo limetokea wakati wa mkutano ulioandaliwa na viongozi wa kidini mjini Nairobi na kuhudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo wanasiasa. Polisi wanasema uchunguzi bado unaendelea na bado hakijajulikana kilichosababisha milipuko hiyo na waliohusuka.

Hata hivyo tayari makundi hasimu yameanza kuelekezeana lawama. Kundi la "NO" linalopinga katiba mpya  linadai kuwa huenda mashambulizi hayo yamelenga kuhujumu mkutano wao na pia kulaumu polisi kwa kutotoa ulinzi wa kutosha kwao. Kutoka Nairobi mwandishi wetu Jason Nyakundi.