Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa Israel dhidi ya tukio la flotilla lazima uwezeshwe kupata ukweli:UM

Uchunguzi wa Israel dhidi ya tukio la flotilla lazima uwezeshwe kupata ukweli:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kukiuka sheria Philip Alston amesema uchunguzi wowote wa Israel dhidi ya tukio la boti ya flotilla Gaza upewe fursa ya kutafuta ukweli.

Amesema bila kuwezeshwa ,uchunguzi huo hautochukuliwa kwa uzito unaostahili.Amesema kuna mambo mengi yanayohitajika ili tume yoyote ya uchunguzi kukidhi viwango vya kimataifa.

Kwanza lazima iwe huru bila mkono wa serikali, pili lazima ipewe uwezo wa kisheria kuweza kupata ushahidi wa pande zote unaohitajika ikiwa ni pamoja na mashahidi muhimu na tatu ripoti yake ya mwisho lazima iwekwe hadharni na sio kwa serikali tuu. Na amesema kama mahitaji yamefikiwa badi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa ukweli wa tukio Fulani.